Wawekezaji waliohudhuria uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji mkoani katavi wametakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji katika mkoa huo wenye zaidi ya hekta 45,000.
Akizungumza katika mkutano huo uliowakutanisha wadau wa uwekeaji kutoka maeneo mbalimbali, Mkuu wa mkoa huo Mhe Juma Homera amesema katika ujenzi wa viwanda mkoa umetenga hekari 245 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda mbalimbali.
“Kutokana na wingi wa samaki wanaovuliwa kutoka ziwa Tanganyika wakiwemo, migebuka, kuhe, sangara pamoja na kamongo, mkoa umetenga hekari 245 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kusindika na kuchakata samaki” Amekakaririwa Homera
Homera ameongeza kuwa wawekezaji wanayo fursa ya ujenzi wa viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya usindikaji nafaka, ujenzi wa viwanda vya asali, uchakataji wa nyama na maziwa, pamoja na viwanda vya mbao.
Katika sekta ya utalii Homera amesema wawekezaji wanayofursa ya kuwekeza katika upande wa makampuni ya utalii yatakayosaidia ongezeko la utalii katika mkoa huo, wenye vivutio vingi va utalii ikiwemo mto mapacha ,mto maji moto pamoja na hifadhi ya taifa katavi yenye ukubwa wa hekari 4471.
“Tuna zaidi ya sokwe 2500, tuna tweiga mweupe ambae huwezi kumpata kokote Tanzania isipokuwa mkoani katavi, lakini pia tunao viboko na tembo wakubwa sana kama nyumba” Amesema
MWISHO
Comments
Post a Comment