Watumishi wa umma popote walipo nchini wametakiwa moja ya kazi zao za msingi iwe ni kuwawezesha na kuwasaidia watu na makampuni yanayotaka kuwekeza kufanya shuhuli zao bila bugudha yoyote.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof. Kitila Mkumbo Mkoani Katavi katika mkutano wa uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji mkoani humo uliowakutanisha wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali.
“Kila siku tunasisitiza, mtumishi wa Umma ukitaka serikali ikuhudumie vizuri, lazima uwaheshimu na kuwathamini wawekezaji na yeyote anaye wanyanyasa na kuwadharau wawekezaji basi hajitambui” Amekaririwa Prof Mkumbo
Aidha, Prof Mkumbo amewataka wananchi kuondoa dhana ya kuwa uwekezaji ni suala linalofanywa na wageni tu, badala yake amewataka watu binafsi na makampuni binafsi na hata wanafunzi wa vyuo vikuu kujitokeza kwa kuwa na mtaji, kufanyabiashara na kupata faida.
“Muwekezaji sio lazima awe ni mtu tajiri sana au kutoka nje ya nchi, La hasha, hata wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali wana uwezo wa kuwa wawekezaji kwa kuweka akiba kutoka kwenye fedha zao za kujikimu na mwisho wa masomo anaweza akawa muwekezaji mkubwa” Amesisitiza
Hata hivyo Prof. Mkumbo pia amewataka wawekezaji kutimiza majukumu yao ya msingi ikiwa ni pamoja na kuwapa stahiki zao ikiwemo mikataba kwa wafanyakazi wao pamoja na kushiriki kujitoa katika huduma za kijamii.
MWISHO
Safi Katabi
ReplyDeleteKatavi
Delete