Na Swaum Katambo, Katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limemkamata Mayala Hinyali (34) ambaye ni mganga wa kienyeji Mkazi wa Kasekese Wilayani Tanganyika kwa kumtorosha mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Usevya kidato cha kwanza jina limehifadhiwa na kwenda kuishi nae kinyumba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Benjamin Kuzaga amethibitisha hayo wakati akizungumza na kituo cha Habari Site Tv na kusema kuwa mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakani kwa hatua zaidi za kisheria.
Kadhalika, Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kukamata mtandao wa watuhumiwa wanaojihusisha na wizi wa pikipiki ambapo Katika msako jeshi la polisi limefanikiwa kukamata jumla ya pikipiki kumi na mbili (12) na watuhumiwa kumi na watano.
Hata hivyo, Kamanda Kuzaga amesema Watuhumiwa hao pamoja na vielelezo vya pikipiki hizo zipo katika kituo cha polisi Mpanda, Huku watuhumiwa wakiendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika majalada hayo yatafikishwa katika ofisi ya Taifa mashitaka mkoa wa Katavi kwa hatua zaidi za kishiria.
Kamanda Kuzaga ametoa mwito kwa wananchi hasa kwa wale walioibiwa pikipiki kufika katika kituo cha Polisi Mpanda wakiwa na viambata vinavyotambulisha pikipiki zao ili kuweza kuzitambua.
Pia, amewataka wananchi kuwa karibu kwa namna ya kushirikiana katika kutoa ushahidi mahakamani hatua stahiki za kisheria kuchukuliwa ili kuweza kutokomeza kabisa wimbi la wahalifu katika Mkoa wa Katavi.
MWISHO
Comments
Post a Comment