Na Swaumu Katambo, Katavi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Abdallah Malela amewaomba watoa mitaji wa huduma za Kibenki kuondoa tabia za Urasimu wa kuwachelewesha kuwapatia mitaji wawekezaji kwani inakwamisha maendeleo ya Nchi.
Ameyasema hayo leo Machi 5, 2020 ofisini kwake wakati akizungumza na Kituo cha Matangazo cha Site Tv kuhusu Matarajio ya Mkoa baada ya kufanyika uzinduzi wa Mwongozo wa Fursa za Uwekezaji Katavi uliofanyika Machi 3, 2020 katika Ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Hata hivyo, Malela amesema kuwa uzinduzi umekuwa na manufaa makubwa kwani wawekezaji 17 walijitokeza siku hiyo huku akiwakaribisha wawekezaji wengine kuendelea kujitokeza kuwekeza katika Mkoa wa Katavi kwa kuwa maeneo bado yapo na fursa nyingi za Uchumi zinapatikana.
Kutokana na malalamiko ya wananchi wengi kuhitaji kitabu hicho cha Mwongozo wa Fursa za Uwekezaji Katavi kupatikana katika lugha ya Kiswahili Malela amesema kuwa Uongozi wa Mkoa wa Katavi una mpango wa kuandaa makala pamoja na nakala zitakazoandikwa kwa lugha za Kiswahili, Kifaransa, Kiarabu n.k
MWISHO
M/MUNGU AZIDI KUWABARIKI WANA KATAVI NA VIONGOZI WAO WOTE WA KATAVI WAZIDI KUWA NA MOYO WA KUSAIDIA NA KULETA MAENDELEO KATAVI NA KWA TANZANIA KWA UJUMLA.. KATAVI OYEEEE.
ReplyDelete