Skip to main content

WATOTO 8,000 MKOANI RUVUMA KUFAIDIKA NA MAFUNZO YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la kuhudumia watu wasiojiweza na wenye Ulemavu (PADI) linatarajia kuanza kutoa mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kiume wenye umri wa miaka tisa hadi 14 katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Meneja Mradi wa PADI Gifti Kilasi amesema kupitia mradi wa USAID KIZAZI KIPYA unnaoratibiwa na PADI,utaanza kutoa mafunzo kwa watoto hao ili waweze kufahamu madhara ya ukatili wa kijinsia na waanze kupinga ukatili huo katika jamii.

Kwa mujibu wa Meneja huyo, Mradi huo umeanza kutekelezwa mwaka 2017 na unatarajia kukamilika mwaka 2021 na kwamba hadi sasa wamesajili watoto 900 wa shule za Msingi na lengo ni kuwafikia watoto 8000 katika Mkoa wa Ruvuma hadi kufikia Septemba 2021.

Ameongeza kuwa wamegeukia kundi hilo kwa sababu ni wahanga wa ukatili wa kijinsi,na kwamba kundi hilo lilisahaulika katika kuwapa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia ukilinganisha na watoto wa kike.

Afisa Ustawi wa Halmashauri ya Wilaya ya songea Suzana Mkondya amewaasa wazazi na walezi kutoa taarifa pale watoto wa kiume wanapofanyiwa vitendo vya ukatili katika jamii. 

Amesema baada ya mafunzo hayo wanatarajia matendo vitendo vya ukatili vitapungua kwa kiasi kikubwa na watoto wataelimika na kuanza kutoa elimu kwa vijana wengine.

Hata hivyo amesema mafunzo hayo yatatolewa kwa nadharia na vitendo kupitia michezo na kwamba yatafundishwa na walimu wa shule za msingi katika maeneo husika na watoto watapata fursa ya kupima afya zao bure.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Zena Ibrahimu ametoa wito kwa wadau wa mradi huo kusimamia vizuri na kutoa ushirikiano wa dhati katika utekelezaji wa mradi huo ili uweze kutoa matokeo chanya ya kujenga na kulinda maadili mema ya kitanzania.

Ibrahimu amewataja Watoto watakaofaidika na mafunzo hayo wanatoka katika Kata za Parangu, Maposeni, Kilagano, Litapwasi, Mpitimbi,Kizuka,Litisha,Magagula,Peramiho na Mbinga mhalule na kwamba kila kata zimechaguliwa shule tatu na kila shule wamechaguliwa wanafunzi 30.

Imeandikwa na Jakline Clavery

Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Songea

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja