Na Jacqelen Clavery -Afisa Habari
Songea DC
Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri hiyo Dr.Erick Kahise ametoa wito huo wakati alipokutana na kufanya kikao na wafugaji katika cha Kijiji cha Nambendo kata ya Ndongosi.
Dr.Kahise amesema usajili wa mifugo utawezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wafugaji kufuatia takwimu sahihi zilizotolewa na wafugaji wenyewe waliopo katika eneo husika.
Dr.Kahise amesema takwimu zitasaidia pia kutenga maeneo ya malisho,ujenzi wa majosho,dawa za uchanjaji wa mifugo,uwekaji wa miundo mbinu na huduma nyingine za kiutalam.
Dkt Kahise ameyataja magonjwa 14 ya kipaumbele ambayo serikali inataka wafugaji kutilia mkazo katika swala zima la chanjo kwa Wanyama wote wanaofugwa.
Amewaagiza wafugaji hao kutokiuka Sheria namba 17 ya mwaka 2003 inayosimamia mifugo kufuata taratibu za kuchanja mifugo kwa sababu chanjo inaboresha afya ya mifugo na kwamba mifugo ikiimarika na uchumi wao pia utaimarika na serikali itakusanya maduhuri,sanjari na kuimarisha lishe katika familia.
“kwa mwaka chanjo itatolewa mara mbili,na bei za chanjo hizo ni bei elekezi ya serikali ambayo haizidi shilingi.1000,na adhabu ya kutochanja mifugo inafikia hadi shilingi 20,000’’,alisema.
Afisa Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Wilaya ya Songea Dr.Erick Kahise akizungumza na wafugaji kuhusu usajiri wa mifugo na sheria za ufugaji katika kijiji cha Nambendo\
Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Nambendo Shaibu Rashidi Makomba amesema mpaka Septemba 15 ,2020 wamesajili wafugaji 17 kati ya wafugaji 115.
Amesema idadi ndogo ya wafugaji waliojitokeza kujisajiri inasababishwa na udanganyifu unaofanywa na wafugaji hao kuficha ukweli kuhusu idadi kamili ya mifugo wanayo miliki.
Ametoa rai kwa wafugaji na wakulima katika Kijiji hicho kushirikiana katika shughuli za maendeleo na kuacha tabia ya kuendekeza migogoro isiyokuwa na tija kwao.
Halmashauri ya wilaya ya Songea imetenga maeneo ya machungio katika kata za Muhukuru Lilihi,Muhukuru barabarani na Ndongosi.
Comments
Post a Comment