Na Mwandishi wetu Site Tv
Mpanda-Katavi
MKUU wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera ametibuka nyongo baada ya Watu aliodai ni waongo kusambaza taarifa za kuwa Uwanja wa Ndege Mpanda Mkoani humo umejaa Nyasi haufanyi kazi.
Akizungumza na Site Tv leo Septemba 17 alipowasili uwanjani hapo kuwapokea Watalii,Homera amekanusha taarifa hizo huku akiwajibu wanaosema hivyo kuwa ni wapotoshaji na hawakuwahi kufika katika Uwanja huo kujionea hali halisi.
"Hawa wanaosema uwanja huu umeota nyasi,nionyeshe masikitiko yangu pengine nyasi zimeota kwenye Miili yao au kwenye Mwili wake. Na Sisi tuko tayari Wananchi wa Katavi kwenda kufyeka hizo Nyasi kwenye Mwili wa huyo Mtu ambaye ameongopa mchana kweupe na Watu wakiwa wanashuhudia"-RC Homera,Katavi.
Baadhi ya abiria kwenye Uwanja wa Ndege Mpanda wakielekea kupanda Ndege kwa ajili ya Safari Aidha,Homera amesema hivi sasa katika uwanja huo vimefungwa vifaa vya kisasa ambavyo vitaziwezesha Ndege kutua muda wowote hata kama ni msimu wa Mvua.
Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege Mpanda Ndg. Jeff Shantiwa amesema kwa sasa Abiria wapo wa kutosha na Ndege inajaa,na amesisitiza kuwa Ulinzi na Usalama katika uwanja huo ni wa kutosha.
Jeff Shantiwa,Meneja Uwanja wa Ndege MpandaKumekuwa na maneno kwenye mitandao ya Kijamii kuwa Ndege zinazofanya safari Mkoani humo hazijai huku wengine wakidai safari zipo mara Moja tu kwa Wiki badala ya mara Tatu kwa Wiki yaani Jumamosi,Jumanne na Alhamisi.
Ndege(Air Tanzania) ikiwa imetua katika uwanja wa Ndege Mpanda Mkoani KataviReplyForward |
Comments
Post a Comment