Wawakilishi wa wazee wa Mkoa wa Ruvuma kutoka wilaya zote tano wakiwa katika kikao maalum cha kuunda Baraza la wazee wa Mkoa pamoja na kuchagua viongozi watakaoongoza Baraza hilo ngazi ya Mkoa wa Ruvuma. Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu akifungua kikao maalum cha uundaji wa Baraza la wazee Mkoa wa Ruvuma na kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi watakaoliongoza baraza hilo ngazi ya Mkoa. Na Albano Midelo Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma Wazee wa Mkoa wa Ruvuma wamefanya kikao maalum cha uundaji Baraza la Wazee la Mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mipango Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea. Waliochaguliwa kuunda Baraza hilo kwenye uchaguzi ulishirikisha wawakilishi kutoka wilaya za Nyasa,Mbinga,Songea,Tunduru na Namtumbo ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa amechaguliwa Elenzian Nyoni kutoka Manispaa ya Songea. Wengine waliochaguliwa ni Lusiana Nduguru kutoka Halmashauri ya Mji wa Mbin...