Na Mwandishi Wetu, Katavi. Wakulima Mkoa wa Katavi wameombwa kuachana na kilimo cha mazoea ambacho hakimkomboi mkulima kiuchumi na badala yake kumfanya kuzalisha mazao ya chakula na biashara yasiyokuwa na tija huku yakimwacha masikini. Kauli hiyo imetolewa jana kwenye ukumbi wa Idara ya Maji Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi na Afsa Masoko na Mauzo wa ETC Agro Tractor,Zahra Salum wakati akizungumza na wadau wa kilimo mkoani humo ambapo aliwaambia kuwa kilimo pekee chenye tija kitamkomboa mkulima kutoka kwenye umasikini. Zahra aliweka wazi kuwa kwa kutambua juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya rais Dkt John Magufuli ya kuadaa sera madhubuti za kuhakikisha sekta ya kilimo inakua kwa kasi na kumfanya mkulima kupiga hatua za maendeleo ya kiuchumi ndio zimeifanya Kampuni ya ETC Agro Tractor kwa kushirikiana na Benki ya CRDB Tawi la Mpanda kuandaa mfumo ambao utamfanya mkulima kupata zana za kilimo za kisasa, ...