Picha ikiwaonyesha Wakurugenzi watendaji,wa Kwanza Kulia ni Bi. Catherine Mashala (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe),wa Pili ni Mohamed Ramadhan (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo),wa Tatu ni Theresia Irafay (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mlele) na wa mwisho ni Sophia Kumbuli (Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda). Wakuu wa Wilaya,kushoto ni Onesmo Buswelu (Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika) na Filberto Sanga (Mkuu wa Wilaya ya Mlele) wakifurahia jambo. Jamila Yusuf,Mkuu wa Wilaya ya Mpanda akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wenzake katika kilele cha wiki ya mwana Katavi na uzinduzi wa msimu mpya wa Kilimo 2022/22. Mwanamvua Mrindoko,Mkuu wa Mkoa wa Katavi akizungumza katika kilele cha wiki ya mwana Katavi na uzinduzi wa msimu mpya wa Kilimo 2022/22. Na Aidan Felson,Site Blog-Katavi. ******************************************** MKOA wa Katavi Jana Nomba 2,2022 umezindua msimu mpya wa Kilimo 2022/23,uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi Kashato Manispaa...