Skip to main content

RC HOMERA ABAINISHA UZINDUZI WA KITABU CHA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI KATAVI

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo tarehe 27 Machi 2020.
Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Katavi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera akisisitiza jambo ofisini kwake leo tarehe 27 Machi 2020.

Mkoa wa Katavi umejipanga kuzindua kitabu cha Uwekezaji “KATAVI INVESTIMENT GUIDE” utakaofanyika katika Ukumbi mpya wa Manispaa ya Mpanda tarehe 3 Machi 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo tarehe 27 Machi 2020.

Amesema kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu hicho anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa huku lengo la uzinduzi wa kitabu hicho ikiwa ni kuhakikisha serikali ya mkoa wa Katavi inakuwa na nyenzo muhimu ya kujenga uchumi.

Homera amesema kuwa kufuatia uzinduliwa  kwa kitabu hicho wawekezaji na wadau mbalimbali watapata fursa ya kuzitambua fursa zilizopo katika mkoa wa Katavi na kuwawezesha wawekezaji katika nyanja mbalimbali itakazokuwa ni lango kuu la uchumi kusini magharibi mwa nchi.

Aidha, Rc Homera amesema kuwa kabla ya siku ya uzinduzi serikali ya mkoa itafanya ziara ya kutembelea sehemu za uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea hifadhi ya Taifa ya Katavi na mwambao wa ziwa Tanganyika ili kujionea vivutio na fursa za uwekezaji.

Ameongeza kuwa tukio la kutembelea vivutio litawafanya wawekezaji kutoka nje ya mkoa kupata fursa ya kukutana na wawekezaji wa ndani ili kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya kiuwekezaji.

Ameitaja kauli mbiu ya uzinduzi huo kuwa ni "Katavi Lango Kuu la Uchumi kusini Magharibi mwa Tanzania; Wekeza Katavi kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda", ambapo kauli mbiu hiyo inalenga kuhamasisha wadau kuwekeza katika Mkoa wa Katavi sambamba na kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania, DRC Congo, Burundi, Rwanda na Zambia.

MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja