Mkulima Mdogo, Emmanuel Ramadhan. Ramadhan Nyembe Mkulima Kijiji cha Majalila. Baadhi ya Wakulima wakivuna Mpunga. Magunia ya Mpunga. PICHA NA ZAINAB MTIMA,Site Tv Na.Swaum Katambo, Tanganyika-Katavi. Licha ya Serikali kuwekeza zaidi ya Bilioni 5 kwa ajili ya Skimu tatu za Umwagiliaji zilizopo Wilayani Mpanda ambazo ni Ugala,Mwamkulu na Uruila,Mkoa wa Katavi hauna Skimu iliyokamilika pamoja na kuwa Mpango wa Serikali wa Mwaka 2021/22 ni kuboresha Kilimo cha Umwagiliaji Nchini. Hayo yanakuja mara baada ya Wakulima katika Kijiji cha Majalila Kata ya Tongwe Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi kusikiliza Hotuba aliyoitoa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Mwigulu Nchemba kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 katika Sekta ya Kilimo kuwa Maeneo yatakayopewa msukumo ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji. "Kwa bajeti iliyosomwa inaonekana wakulima inatuinua,Serikali imetuangalia kwa macho mawili labda tusubiri utekelezaji kwa sababu yanayosemwa ni mazuri...