Na Swaum Katambo, Mpanda-Katavi Jumla ya Wahitimu 40 wa Mafunzo ya Huduma ya kwanza yaliyotolewa na Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross) Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametunukiwa Vyeti baada kushiriki Mafunzo ya takribani Siku 10 yaliyoanza Oktoba 5 na kumalizika Oktoba 16 katika Ukumbi wa Serena uliopo Kata ya Makanyagio. Akihitimisha Mafunzo hayo katika hafla iliyofanyika kwa Wahitimu wa Mafunzo hayo Mgeni rasmi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Omary Sukari,amepongeza hatua ya Red Cross Tanzania kuona umuhimu wa kutoa mafunzo hayo kwa Wanakatavi kwani kabla ya mafunzo hayo Mkoa mzima ulikuwa na Watu Watatu tu waliopata mafunzo hayo kiusahihi huku akiahidi kuwa Sekta ya Afya ipo tayari kutoa vifaa maalum vya huduma ya kwanza kwa shirika la red Cross Mkoani Katavi kutokana na uwepo wa uhaba wa Vifaa. Dkt. Sukari pia ameahidi kuandika barua zitakazozifikia Taasisi zote zilizopo Mkoani humo ili kuhakikisha Elimu ya Huduma ya kwanza (Red Cross) inatolewa kwa Wat...