Skip to main content

WAKULIMA NZEGA WAPO TAYARI KWA UJENZI NA UKARABATI WA MRADI WA UMWAGILIAJI IDUDUMO.

Kulia, Mhandisi Mwinchuma Tengeneza akimkabidhi kablasha la eneo la kazi ya Ujenzi na Ukarabati wa miundombinu, katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Idudumo mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya Explicit Main Constructors Ltd Bw. Basil Clement (kushoto).


Picha Ikionesha eneo la Utoro wa Maji katika Bwawa la Idudumo ambalo litavyunjwa na kunjengwa upya.

Wa pili kutoka kulia, Meneja Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Skimu ya Umwagiliaji Idudumo Bw. Juma Kibori akiwaonesha wawakilishi wa viongozi wa Halmashauri ya Nzega mji na wataalam ramani ya ujenzi na ukarabati wa neo la mradi.


Picha ikionesha sehemu ya eneo la Bwawa Idudumo, ambalo litafanyiwa ukarabati katika awamu nyingine ya mradi.

                ************************************************

                                    Na; Mwandishi wetu - Nzega

Wakulima katika Halmashauri ya mji wa Nzega Mkoani Tabora, wameonesha kuwa tayari na kutoa ushikiano kwa ujenzi na ukarabati wa mradi wa kilimo cha Umwagiliaji Idudumo unaofadhiliwa na Serikali kwa silimia mia.

Wakiongea kwa nyakati tofauti katika makabidhiano ya eneo la kazi katika skimu hiyo, Bw. Pascal Maganga ambaye ni mkulima wa zao la mpunga katika skimu hiyo alisema, ujenzi na ukarabati wa miundombi katika skimu hiyo utasaidia wakulima kulima zaidi ya mara moja katika misimu tofauti ya mvua, tofauti na sasa ambapo ukosekanaji wa miundombinu unapelekea mashamba kujaa maji na kutokulima kwa wakati na kuweza kuleta madhara kwa mazao.

“Naamini kuwa baada ya ujenzi na maboresho haya, kwa heka awali mkulima kama alikuwa anapata gunia thelathini (30) ila baada ya maboresho haya tutavuna zaidi .” Alisee Mkulima hiyo.

Akiongea wakati wa makabithiano hayo, Meneja mradi huo Mhandisi Juma Kibori kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alisema, eneo la skmu hiyo ya kilimo cha Umwagiliaji yenye ukubwa Hekta 300, na kujikita zaidi katika kilimo cha mpunga lenye chanzo chake cha maji ya Bwawa la Idudumo, lilikuwa likitumia njia za asili na sasa itajengewa mfereji mkubwa wa kupeleka maji mashambani wenye urefu wa mita 1500, vigawa maji sita, makaravati matano na mifereji ya upili yenye urefu wa mita zaidi ya mia sita.

Aliendelea kusema kuwa, awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi na ukarabati wa skimu hiyo utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 700, unaotegemea kuchukua miezi nane, utaboresha miundombinu na kusaidia wakulima kuwa na kilimo cha uhakika.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja