Skip to main content

UNHCR YAKABIDHI MISAADA KWA MAHABUSU MPANDA.

Na.Swaum Katambo
Site Tv - Mpanda

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR leo Feb 18 limekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali katika Gereza la Mahabusu Mpanda kama sehemu ya wadau muhimu katika kuwahudumia watanzania na wasio watanzania (wakimbizi).

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Afisa Hifadhi mwandamizi Bw.Peter Muriuki kutoka Shirika la UNHCR Kigoma amesema wanatambua kwamba Magereza ni mdau muhimu sana kwa shughuli za haki, usalama na kurekebisha tabia.

"Mara kwa mara wakimbizi wamejikuta katika changamoto za kuhukumiwa, na Shirika la UNHCR linakuja kuwafuata na kuwatafuta magerezani kuwajulia hali waliyonayo huku, na kama wako na mahitaji ambayo tunaweza kuyatimiza tukishirikiana na Idara ya magereza"Alisema Bw.Muriuki.
Bw.Peter Muriuki Afisa Hifadhi mwandamizi Shirika la UNHCR Kigoma

Hata Hivyo ameongeza kuwa wanatambua kuwa magereza wanatoa huduma iliyo na usawa kwa mahabusu walio wazawa na wageni ambao ni wakimbizi hivyo mchango wao haulengi wakimbizi pekee.

"Tunawaachia idara yenyewe kama vile inavyowahudumia wateja walio nao bila kuwabagua pia waamue kutoa huo mchango kwa sababu tuna uhakika kwamba utawafikia wakimbizi na wafungwa wengine",Aliongeza.

Nae Rehema Msami kutoka Shirika hilo la UNHCR amebainisha vifaa walivyo kabidhi kama msaada katika Gereza hilo ambavyo ni Magodoro 80, Blanketi 120, Ndoo 200, Mafuta ya kupakaa pisi 200, Dawa za Meno na miswaki 200, dawa za kuzuia Mbu 200, Viatu aina ya Yeboyebo 200, Sabuni Miche 240, Taulo za kike 50,  na Khanga doti 50.
Rehema Msami akibainisha vifaa walivyokabidhi

Kwa upande wake Mrakibu Msaidizi wa Magereza katika Mahabusu  ya Mpanda ASP Khalfan Tangila kwa niaba ya Mkuu wa Gereza ameshukuru msaada waliopokea ambapo amesema kuwa vitu walivyopokea vilikuwa katika sehemu ya changamoto walizokuwa nazo mahabusu hapo.
Mrakibu Msaidizi wa Magereza Mahabusu  ya Mpanda ASP Khalfan Tangila akitoa shukrani

"Hii imetufanya tuwe vizuri kwa sababu kuna vitu ambavyo hatukuwa navyo lakini UNHCR wameona kwamba kuna sababu ya kutuletea, mfano Magodoro,dawa za meno na vitu vingine",Alisema ASP Tangila

Hata hivyo amewaomba wadau hao wasiache kuendelea kutoa misaada na kutembelea katika Gereza hilo ili kuona mapungufu mengine ambayo wanaweza kuwasaidia.

MWISHO.


Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja