Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda,Mhe.Haidary Sumry akizungumza na wanak ikundi cha Watu wenye ulemavu (Tujiendeleze). ******************************************************** "Mkopo tuliopata kutoka Halmashauri, umetuwezesha kupunguza ukali wa maisha ambapo kwasasa familia zetu zina uwezo wa kula Milo mitatu kwa siku ukilinganisha na hapo awali" Na.Swaum Katambo Mpanda-Katavi Ni wajibu uliowekwa na sheria kwa Serikali za Mitaa kutenga asilimia kumi ya mapato yanayokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani vya mapato kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vilivyosajiliwa vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu. Mwongozo huu unaelezea kwa lugha nyepesi kanuni zilizowekwa chini ya sheria ya fedha ya serikali za mitaa chini ya kifungu cha 37 ambazo zinajulikana kama kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya wana...