Pichani Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani, Ofisini kwake jijini Dodoma mapema leo, kuhusu Mafanikio katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji ndani ya kipindi cha miaka sitini ya uhuru. Na,Mwanshi Wetu. Kuhusu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji; Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sera ya umwagiliaji ya Taifa ya Mwaka 2010, ilitoa Mwongozo wa kuwepo kwa mambo mahususi kwenye uendelezwaji wa sekta ya Umwagiliaji pamoja na mambo mengine ni kuwa na chombo cha kuboresha na kusimamia sekta ya umwagiliaji nchini. Kilimo cha umwagiliaji kilianzia mkoani Arusha enzi za ukoloni, na baada ya Uhuru serikali iliendeleza mikakati mbalimbali ndipo mipango mahuhusi ilianzishwa chini ya wizara husika kama Wizara ya maji na kilimo. Ameeleza Bwana Daudi Kaali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Akiongea Ofisini kwake Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Godwin Mutahangarwa, alisema kat...