Skip to main content

SERIKALI IMETOA WITO KWA WASANII NCHINI KUENDELEA KUSAJILI KAZI ZAO KATIKA MAMLAKA ZINAZO HUSIKA ILI ZILINDWE KISHERIA.


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akijibu maswali ya baadhi ya wabunge wakati wa kikao kati ya watendaji wa Wizara yake na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 25, 2021 Bungeni jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Aloyce  Kamamba akisisitiza jambo wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Oktoba 25, 2021 Bungeni jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizira ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Oktoba 25, 2021 Bungeni jijini Dodoma.




Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Oktoba 25, 2021 Bungeni jijini Dodoma.



Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii katika kikao na  watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Oktoba 25, 2021 Bungeni jijini Dodoma.

                            ****************************************

                            Na: Projestus Binamungu,Dodoma.

                                             25/10/2021

Serikali imetoa wito kwa wasanii kuendelea kusajili kazi zao katika mamlaka zinazo husika ili zilindwe kisheria na malaka hizo katika kuhakikisha zinawanufaisha na kufanikisha ndoto zao.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa wakati akijibu maswali ya baadhi ya Wabunge waliotaka kujua msimamo wa Serikali katika kuthibiti wizi wa kazi za Sanaa kupitia ombwe kubwa la uwepo wa teknolojia zinazo wawezesha wezi kudurufu kazi za wasanii na kuziuza bila kibali cha msanii husika.

Katika kikao hicho baina ya watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii, Waziri Bashungwa amewaelezea wajumbe kuwa nia ya Serikali ni kuona vijana wananufaika kupitia kazi zao , lakini kwa kufuata Sheria za nchi, Kanuni, Taratibu na Miongozo zilizowekwa kwa lengo la kulinda masilahi yao.

“Kwa hiyo ndugu zangu wajumbe tuendelee kusaidizana kuwahimiza hawa vijana wetu kila mmoja kwa nafasi yake kwamba ni muhimu kusajili kazi zao, ili linapotokea suala la kuibiwa kazi tuwe na meno na sehemu ya kuanzia kisheria katika kufuatilia haki ya msanii husika” amesema Waziri Basungwa mbele ya kamati hiyo ya Bunge.

Awali Katibu Mkuu wa Wizira ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Wizara hiyo inaendelea na uratibu kuona namna bora inavyoweza kuwapeleka wataalamu wa sanaa nje ya nchi kujifunza na kuongeza ujuzi zaidi ili baadae warejee hapa nchini kuwasaidia wasanii na hasa wasanii wachanga kuzalisha kazi zenye ubora zaidi.

Akizungumza kabla ya kuhairisha kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Aloyce  Kamamba amepongeza hatua zinazo fanywa na Wizara ya Utamadunia, Sanaa na Michezo ikiwa ni pamoja na hatua ya kuwezesha kutengwa kwa asilimia tano ya mapato kutoka kwenye michezo ya kubahatisha ambayo inaiwezesha Wizara kupata fedha kiasi cha shilingi Milioni 400 kwa kila robo ya mwaka kutokana na asilimia hiyo.

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja