Skip to main content

RC MKOA WA RUVUMA AZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA MBOLEA DUNIANI.


KUSHOTO KATIKATI NI MKUU WA MKOA WA RUVUMA BRIGEDIA JENERALI WILBERT IBUGE AKIKAGUA MOJA KATI YA VIBANDA 41 VYA MAONESHO YA MAADHIMISHO SIKU YA MBOLEA DUNIANI AMBAY KITAIFA MWAKA HUU  YANAFANYIKA UWANJA WA MAJIMAJI MJINI SONGEA KUANZIA OKTOBA 11 HADI 13.


KUSHOTO NI MKUU WA MKOA WA RUVUMA BRIGEDIA JENERALI WILBERT IBUGE AKISALIMIANA NA  WAKUU WA WILAYA ZA MKOA WA RUVUMA MARA BAADA YA  KUINGIA KWENYE UWANJA WA MAJIMAJI MJINI SONGEA KWA AJILI YA KUZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA MBOLEA DUNIANI.

                ************************************************

                                Na Mwandishi Wetu,Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge Jana Oktoba 11,2021 alizindua maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani yaliyofanyika katika Uwanja wa Majimaji Mjini Songea.

Kabla ya kuzindua maonesho hayo RC Ibuge alikagua vibanda 41 vya washiriki wa maonesho ambayo yanafanyika kuanzia Oktoba 11 na kilele chake ni Oktoba 13.

Akizungumza na wananchi kwenye uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,amesema Mkoa una chakula cha kutosha kwa muda mrefu ambapo katika msimu wa mwaka 2020/2021,Mkoa wa Ruvuma umezalisha tani 1,384,705 za mazao yote ya chakula na kuwa na ziada ya tani 894,960.

‘’Kwa zao la mahindi pekee uzalishaji ni tani 816,242 hivyo kuwa na ziada ya jumla ya tani 326,497 za mahindi’’,alisisitiza RC Ibuge.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,amesema uzalishaji huo unaambatana na matumizi ya pembejeo bora ikiwemo mbolea .

Ameyataja mahitaji ya mbolea katika Mkoa wa Ruvuma kuwa ni jumla ya tani 50,521 kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2020/2021 ambapo mbolea zilizoingia na kutumika ni tani 43,000 na kwamba katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022 Mkoa unatarajia kutumia mbolea tani 50,521 za aina zote za mbolea.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt.Stephano Ngailo ameutaja mkakati mkuu wa serikali ni kuhakikisha kuwa mbolea inapatikana kwa wingi na bei nafuu kwa kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya mbolea hapa nchini.

Amesema serikali imeanza ujenzi wa kiwanda cha mbolea mkoani Dodoma ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mbolea za aina mbalimbali zaidi ya tani laki sita kwa mwaka.

Dkt.Ngailo amesema kiwanda hicho kinatarajia kuanza uzalishaji msimu wa mwaka 2022/2023, ambacho amesema kitakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wakulima hapa nchini wakiwemo wa Mkoa wa Ruvuma ambao wanaongoza kwa kuzalisha mazao ya chakula nchini.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya mbolea duniani ni tumia mbolea bora, kwa tija na kilimo endelevu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 11,2021

Comments

Popular posts from this blog

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja

Katavi Yakemea Vikali Ushoga,Mauaji "Wanaume Msiwazuie Wake Zenu Kufanya...