Skip to main content

WAKULIMA WANUFAIKA NA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MOMBO.


Picha ikionesha sehemu ya shamba la mpunga katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Mombo.


Picha ikionesha Mfereji wa upili unaopeleka maji mashambani katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Mombo.

                                ******************************

                                    Na; Mwandishi Wetu - Mombo

Wakulima katika siku ya kilimo cha Umwagiliaji Mombo Wilayani Korogwe, wamenufaika na Kilimo hicho baada ya Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuwajengea miundombinu inayopeleka maji mashambani pamoja na kuwajengea maghala ya kuifadhia mazao,kupata elimu ya kuongeza thamani ya zao la mpunga linalolimwa katika katika skimu hiyo pamoja na elimu ya mafunzo na matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika skimu hiyo baadhi ya wakulima wamesema kuwa, kupitia kuwepo kwa miundombinu thabiti katika mashamba hayo, wameweza kulima kilimo cha teknolojia mpya, na kuongezeka kwa pato la mkulima mmoja mmoja, kujenga na kuishi katika nyumba za kisasa pamoja na kumudu kuwapeleka watoto shule.

Bwana Hamis Said mwenyekiti wa ushirika wa wakulima katika skimu hiyo alisema sambamba na faida wanayoipata kutokana na kilimo katika skimu hiyo wameweza kupata elimu kuhusu uchangiaji wa ada za huduma ya umwagiliaji pamoja na utekelezaji wake.

Skimu ya Kilimo cha umwagiliaji Mombo ina ukubwa wa eneo la hekta 220, zinazotumika katika kilimo cha umwagiliaji katika misimu miwili kwa mwaka yaani kiangazi na vuli ambapo jumla ya wakulima 429 wanajishughulisha katika shuguli za kilimo cha umwagiliaji.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja