Skip to main content

DKT. KIJAJI AIKUMBUSHA MENEJIMENTI YA WIZARA YAKE KUTEKELEZA WAJIBU.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na
Menejimenti ya Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba mara baada ya kuapishwa Ikulu ya
Chamwino jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wake, Mhandisi Kundo Mathew na kushoto
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula.


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew
(kushoto) akizungumza mara baada ya Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji (aliyeketi)
kupokelewa na kuzungumza na Menejimenti ya Wizara hiyo Mji wa Serikali Mtumba mara
baada ya kuapishwa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Dkt. Zainab Chaula.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula
akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto kwake) na
Menejimenti ya Wizara hiyo mara baada ya kuapishwa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Anayefuata baada ya Dkt. Kijaji ni Naibu Waziri wake Mhandisi Kundo Mathew.


Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO, Gerson Msigwa
akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari baada ya kikao cha Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji na
Menejimenti hiyo kilichofanyika Mji wa Serikali Mtumba mara baada ya kuapishwa Ikulu ya
Chamwino jijini Dodoma.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji (aliyeketi kushoto)
na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa wakiwa katika picha ya pamoja
na Naibu Mawaziri wa Wizara hizo, Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Mkuu baada ya
kupokelewa na Menejimenti ya Wizara hizo katika Ofisi zao zilizopo Mji wa Serikali Mtumba
baada ya kuapishwa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kulia) akipokelewa na Naibu Waziri wake Mhandisi Kundo Mathew (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula (wa pili kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kushoto) alipowasili Wizarani hapo kwenye Mji wa Serikali, Mtumba baada ya kuapishwa Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

                    *************************************

                    * Asema Tuko Hapa Kuwatumikia Wananchi

                       Na,Prisca Ulomi na Faraja Mpina, DODOMA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Ashatu kijaji ameitaka Menejimenti na watumishi wa Wizara yake itambue kuwa lengo na dhumuni la kuundwa kwa Wizara hiyo ni kuwatumikia wananchi kwa kutekeleza kile kilichoelekezwa kwenye Ilani ya CCM ya 2020-2025 kwa kuzisoma na kuziishi kurasa zinazohusu Wizara hiyo.

Hayo ameyazungumza Dkt. Kijaji katika kikao chake cha kwanza na Menejimenti ya Wizara hiyo kilichofanyika katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu ya Chamwino,Dodoma.

Dkt. Kijaji amesema kuwa watendaji wa Wizara hiyo wanatakiwa kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi mkubwa kwa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kwa sababu umma wa watanzania una uchu wa kusikia kinachoendelea duniani hivyo kabla ya kufungia chombo chochote cha habari ni vema kutekeleza wajibu kwanza.

“Mifumo yote ya Taifa hili ipo chini ya Wizara hii na tumeunganishwa na Sekta ya Habari,twendeni tukahakikishe tunafanya kazi kwa matokeo yanayoonekana”, Amesema Dkt. Kijaji

Amesema kuwa matarajio yake ni kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na upendo baina ya viongozi wa Wizara hiyo bila kusuguana kwa kufuata utaratibu wa utumishi wa umma ikiwemo kutunza siri za Serikali na kutoa taarifa sahihi kwa umma.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa maelekezo aliyoyatoa Waziri wake yamelenga kufanya kazi kwa matokeo yanayohitajika ili baadae yaoneshe mabadiliko katika jamii wanayoitumikia na kuahidi kuwa yeye binafsi pamoja na Menejimenti nzima ya Wizara hiyo imepokea maelekezo hayo na inaenda kuyafanyia kazi kwa ufanisi mkubwa

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula aliitambulisha Menejimenti ya Wizara hiyo akiwemo Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO baada ya Sekta ya Habari kumegwa kutoka Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo na kuhamishiwa kwa iliyokuwa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kuunda Wizara mpya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Chaula amesisitiza menejimenti hiyo kuendelea kufanya kazi kwa kufuata Sheria,taratibu na kanuni za utumishi wa umma ili matokeo ya kazi na majukumu ya kila mmoja wao iwe yenye tija na ufanisi mkubwa

Naye Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO, Gerson Msigwa kwa niaba ya Menejimenti hiyo amesema kuwa wamepokea maelekezo ya Waziri huyo na kuahidi kuwa watii, wasikivu na kuchapa kazi kwa kiwango ambacho kimetolewa muongozo na kiongozi huyo.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja