Skip to main content

UCSAF YAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE YA SEKONDARI DUTWA NA NKOLOLO.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kulia) akikabidhiwa kompyuta na Mkuu wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) (aliyevaa barakoa) wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya ya Bariadi Mhe. Lupakisyo Kapange.



Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew na Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange wakikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Shule ya Sekondari
Dutwa anayepokea ni Mwalimu wa shule hiyo Mekrina Bonifasi.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (mwenye miwani), akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nkololo alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa ajili ya shule hiyo.


Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nkololo wakifurahia ugeni uliofika shuleni hapo
ukiongozwa na Mbunge wa Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari Mhandisi Kundo Mathew (hayupo pichani) kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA kwa
ajili ya shule hiyo ambavyo ni printa 1 na Kompyuta 5.

                        *****************************************

                                        Na Faraja Mpina,SIMIYU

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imekabidhi vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya Shule ya Sekondari Dutwa na Shule ya Sekondari Nkololo zilizopo katika Wilaya ya Bariadi ambavyo ni kompyuta 10 na printa 2 ambapo kila shule imepatiwa kompyuta 5 na pinta 1.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Mbunge wa Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew ambaye ndiye aliyevikabidhi katika shule hizo akiambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Lupakisyo Kapange.

“TEHAMA inaenda kuchangia kukuza uchumi wa dunia na sisi Tanzania tumeona kwamba tusibaki nyuma katika kukuza matumizi ya TEHAMA kwa kuhakikisha vijana wetu wanajifunza TEHAMA kuanzia shuleni na nikiwa kama Mbunge wa Bariadi nina kila sababu ya kuwasisitiza vijana wetu kusoma kwa bidii”, amezungumza Mhandisi Kundo

Naibu Waziri huyo ametoa rai kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kupata ufaulu mzuri katika mitihani yao ya Kitaifa na kusisitiza kuwa wanafunzi watakaopata ufualu wa daraja la kwanza la pointi 7,8,9 atawalipia ada kama alivyoahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka 2020

Ameongeza kuwa mpaka sasa amekwishawalipia ada wanafunzi 18 wa kidato cha tano ambao wamepata ufaulu huo katika matokeo ya mwaka huu na wale ambao wamefaulu lakini familia zao zimethibitishwa kuwa hazina uwezo wa kuwaendeleza

Kwa Upande wa Mkuu wa Uendeshaji wa UCSAF Eng. Albert Richard amesema moja ya majukumu yanayotekelezwa na Mfuko huo ni kupeleka vifaa vya TEHAMA katika shule za umma ili kuendelea kuinua matumizi ya TEHAMA nchini.

Naye Mwalimu Mekrina Bonifasi wa Shule ya Sekondari Dutwa amesema kuwa msaada huo wa kompyuta utakuwa chachu ya ufaulu na utasaidia sana katika ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi hasa ukizangatia kuwa kwa sasa shule hiyo ina wanafunzi wa kidato cha kwanza wapatao 280 ambao wanasoma somo la kompyuta na watafanya mtihani wa Taifa 2022 kwa mara ya kwanza.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo ambaye pia ndiye Mbunge wa Bariadi amesikitishwa na uongozi mzima wa Kata ya Nkololo kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa maabara ya TEHAMA katika shule ya Sekondari Nkololo wakati tayari Mbunge huyo alikwishapeleka mifuko 156 ya simenti na mabati 50 toka mwezi Machi, 2020 lakini mpaka sasa hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya kufyatua tofali 1500.

Ameongeza kuwa, mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuja kuulizwa kimetekeleza nini wakati jitihada zinafanyika za kuleta nyenzo za kutekeleza yale ambayo yameandikwa kwenye Ilani ya Chama hicho ambayo ndani yake imeongelea masuala ya TEHAMA lakini bado viongozi wa Chama na Serikali katika ngazi ya Kata hiyo wameshindwa kusimamia utekelezaji wa yale yaliyokusudiwa

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Lupakisyo Kapange amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri na Wataalam wake wahakikishe wanatoka ofisini na kwenda kuweka kambi katika shule hiyo ili kusimamia ujenzi wa darasa hilo hadi ukamilike

“Baada ya hapa nataka nipate maelezo kwanini darasa halijakamilika kutoka mwezi Machi mpaka sasa na wakati vifaa vyote vipo, nani alikuwa anasimamia, nani alipinga na nani alichelewesha na taarifa hiyo niipate ndani ya wiki moja” alizungumza Mhe. Kapange

Aidha, iliamuliwa kuwa vifaa vya TEHAMA vilivyopelekwa kwa ajili ya Shule ya Sekondari Nkololo vihifadhiwe na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mpaka hapo chumba cha maabara ya TEHAMA ya shule hiyo kitakapokamilika ndio.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...