Skip to main content

MFUMO WA STAKABADHI GHALANI WAWAINGIZIA WAKULIMA ZAIDI YA BILIONI 65.


Moja ya Minada ya zao la Soya kupitia Mfumo wa Stakabadhi ghalani uliofanyika eneo la Lilambo Wilayani Songea.


Kushoto mwenye Suti Nyeusi ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mkongogulioni Wilaya ya Namtumbo kuhusu umuhimu wa kuuza Mazao kwa mfumo wa Stakabadhi ghalani.

                         ***************************************

                                    Imeandikwa na Albano Midelo

                                    Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye mazao umewawezesha wakulima Mkoani Ruvuma,kujipatia zaidi ya shilingi bilioni 65 kupitia mazao ya ufuta,mbaazi na soya.

Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Ruvuma Bumi Masuba amesema katika misimu mitatu ya kilimo kuanzia 2018/2019 hadi kufikia msimu wa 2020/2021,Mkoa wa Ruvuma kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ulikusanya kilo 27,664,631 na kuwawezesha wakulima kupata kiasi hicho cha fedha.

“Katika msimu wa mwaka 2020/2021 pekee jumla ya minada 29 ya ufuta imefanyika ambapo jumla ya kilo 8,326 za ufuta ziliuzwa kwa wastani wa bei ya shilingi 2,183 za kilo na kuwapatia wakulima jumla ya shilingi bilioni 17,221,852,087’’,alisema Masuba.

Akizungumzia kuhusu zao la soya,Masuba amesema katika kipindi cha misimu mitatu kuanzia mwaka 2018/2019 hadi 2020/2021 jumla ya kilo 4,963,088 za soya zilikusanywa na kuuzwa kwa wastani wa bei ya shilingi 3,375 kwa kilo na kuwaingiza wakulima shilingi 5,234,096,169.00.

Hata hivyo amesema katika msimu wa mwaka 2020/2021 pekee jumla ya minada tisa ya soya imefanyika ambayo imewezesha kuuza kilo 1,090,199 za soya zilizouzwa kwa wastani wa bei shilingi 1,327 na kuwapatia wakulima jumla ya shilingi 1,547,202,688.00 na kwamba ununuzii unaendelea.

Kuhusu zao la mbaazi,Mrajisi huyo wa Ushirika amesema katika kipindi cha misimu mitatu mfululizo ya kilimo kutoka mwaka 2019/2020 hadi 2020/2021,jumla ya kilo 5,864,615 za mbaazi zilikusanywa na kuuzwa kwa wastani wa bei ya shilingi 2,491 na kuwapatia wakulima jumla ya shilingi 3,779,134,182.

Hata hivyo amesema katika msimu wa mwaka 2020/2021 pekee imefanyika minada mitatu yenye jumla ya kilo 808,295 za mbaazi zilizouzwa kwa wastani wa bei ya shilingi 1,252 kwa kilo na kuwapatia wakulima shilingi 1,011,711,013 na kwamba ununuzi unaendelea. 

Mfumo wa stakabadhi ghalani mkoani Ruvuma umekuwa ni msaada mkubwa kwa kuwapatia wakulima kipato kikubwa unapotekelezwa ipasavyo kulingana na miongozo.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja