Skip to main content

SHERIA MPYA YA MADINI YAPELEKEA TANI 508.9 KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI

Na Swaum Katambo-Katavi

Sheria mpya ya Madini ya uongezaji thamani madini chini ya kifungu cha 129 iloyopitishwa Agosti 28, 2020 inayoruhusu kusafirisha Makinikia nje ya Nchi yenye kiwango cha shaba kisichopungua asilimia 20 imesaidia kusafirisha Tani 508.9 za makinikia kutoka mgodi wa Katavi Mining Co.Ltd kwenda nje ya Nchi kwa mara ya kwanza.

Meneja wa Mgodi wa Katavi Mining Company Ltd Ndg Twalib Mohamed Seif ameyasema hayo leo tarehe 2 Machi 2021 wakati akitoa taarifa ya mgodi huo mbele ya Waziri Wa Nchi Ofisi Rais Uwekezaji Prof. Kitila Alexandra Mkumbo alipotembelea Kiwandani hapo na kubainisha kuwa jumla ya malipo yanayotokana na usafirishaji wa kwanza wa Makinikia ya Shaba ni kiasi cha Shilingi za kitanzania 449,251,452.22

Hata hivyo Twalib ameiomba Serikali iwapatie umeme wa uhakika ili kupunguza gharama za uzalishaji kwani kwa sasa wanatumia Jenereta kwa shughuli za uwezeshaji Mgodi.

Pia ameiomba Serikali kusaidia kutengeneza barabara yenye urefu wa Km 8 kutoka barabara kuu iendayo Sumbawanga hadi eneo la mgodi.

Kadhalika Seif ameiomba Serikali kupitia Ofisi ya Madini Mpanda mkoani Katavi kuwapatia Mwongozo na usimamizi ili kuweza kufanikisha ununuzi wa Malighafi kutoka kwa wachimbaji wadogo.

Kuhusu barabara, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera  amesema kuwa ili kutatua Changamoto hiyo serikali inaendelea kulifanyia kazi ambapo kwa ushirikiano na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) itatengenza.

Pia ameupongeza uongozi wa Katavi Mining Company Ltd kwani uwekezaji wao unaingizia Halmashauri kipato.

Kwa upande wake Waziri Wa Nchi Ofisi Rais Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo ameupongeza uongozi wa Katavi Mining Company Ltd kwa kufanya kazi nzuri huku akiitambua changamoto kubwa ya upatikanaji wa Umeme unaozikabili Kampuni za uwekezaji Mkoani Katavi hadi kupelekea kushindwa kufanya vizuri shughuli za uwekezaji.

Akizungumza na Mwekezaji wa Mgodi wa Katavi Mining Company Ltd Eng. Mahmoud Abdulrazack, Waziri Mkumbo amepongeza Sheria ya Madini ya Mwaka 2017 na Kanuni zake na kusema kuwa baada ya Sheria hiyo wawekezaji wengi wa sekta ya Madini kutoka nchini Oman wamependezwa na uwekezaji nchini Tanzania.

MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja