Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo tarehe 27 Machi 2020. Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Katavi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera akisisitiza jambo ofisini kwake leo tarehe 27 Machi 2020. Mkoa wa Katavi umejipanga kuzindua kitabu cha Uwekezaji “KATAVI INVESTIMENT GUIDE” utakaofanyika katika Ukumbi mpya wa Manispaa ya Mpanda tarehe 3 Machi 2020. Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo tarehe 27 Machi 2020. Amesema kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu hicho anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa huku lengo la uzinduzi wa kitabu hicho ikiwa ni kuhakikisha serikali ya mkoa wa Katavi i nakuwa na nyenzo muhimu ya kujenga uchumi . Homera amesema kuwa kufuatia uzinduliwa kwa kitabu hicho wawekezaji na wadau mbalimbali watapata fursa ya kuzitambua fursa zilizopo katika mkoa wa Katav...