Skip to main content

RC KUNENGE AMTAKA MKANDARASI WA UJENZI WA BARABARA YA TEGETA NYUKI KUKAMILISHA UJEZI IFIKAPO MWEZI OCTOBER, ASEMA ENDAPO ATAKAIDI "PATACHIMBIKA".

Na Mwandishi wetu,


Dar Es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Aboubakar Kunenge ametoa mwezi mmoja kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa barabaara ya Tegeta Nyuki yenye urefu wa Kilometa 1.06 kuhakikisha anakamilisha kwa wakati  na kueleza kuwa endapo atashindwa kutekeleza agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

RC Kunenge ametoa maagizo hayo wakati Wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo amesema mkandarasi huyo wa Kampuni ya CMG Construction amekuwa akisuasua kumaliza mradi licha ya kuongezewa muda ambapo amewaelekeza TARURA kumsimamia ipasavyo Mkandarasi huyo.

Aidha RC Kunenge pia ametembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa Stand Mpya ya kisasa Mbezi Louis ambayo ujenzi wake umefika 80% na inagharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 56 ambapo ameonyesha kuridhishwa na hatua ya ujenzi ilipofikia.



Akiwa kwenye ukaguzi wa Barabara ya Madale - Wazo yenye urefu wa Km 6 inayogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 9.9, RC Kunenge amefurahishwa na juhudi za mkandarasi huyo huku akieleza kuwa barabara hiyo ikikamilika itakuwa "shortcut" nzuri ya kutoka Mbezi kupitia Madale hadi Wazo.

Katika ziara hiyo RC Kunenge pia ametembelea ujenzi wa Daraja la Ulongoni A lililopo Kata ya Gongolamboto ambalo ujenzi wake unagharimu Shilingi Bilioni 4.3 na Ujenzi wa Daraja la Ulongoni B ambapo amewahimiza wakandarasi kuongeza juhudi ili ujenzi ukamilike ndani ya Muda uliopangwa ili kupunguza kero walizokuwa wakizipata wananchi.



Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja