Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2020

APATWA NA MAUTI KWA KUPIGWA NA RADI AKIENDESHA PIKIPIKI BARABARANI.

 Na Mwandishi Wetu.          Katavi. MTU   mmoja   Mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hotel  katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi aliyejulikana kwa jina la  Paulo  Chundu   amekufa hapo hapo baada ya kupigwa na radi akiwa anaaendesha pikipiki wakati akitokea kwenye shamba la mpunga .  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Benjamin  Kuzaga aliwaambia wandishi wa habari kuwa tukio la kifo cha marehemu huyo  lilitokea hapo juzi majira ya saa 12  jioni katika eneo la  Kalilankuluku Tarafa ya Kabungu Wilaya ya Tanganyika .  Kuzaga alieleza kuwa kabla ya tukio hilo marehemu huyo alikuwa ameaga nyumbani kwake kuwa anapeleka chakula  kwenye shamba lake la mpunga kwa ajiri ya chakula  cha vibarua waliokuwa wakifanya kazi kwenye shamba hilo .  Baada ya kuwa ameaga nyumbani kwake marehemu huyo alipakia chakula hicho kwenye pikipiki  yake na kuelekea kwenye shamba hi...